Neno haki ni neno pana kwenye ulimwengu wa sheria lilo na maana na ushahili halali wa mtu bila upendeleo wa aina yoyote,Hta hivyo wengine hufafanua kuwa haki pasipo na wajibu ni upendeleo pia kwa misingi hiyo ni lazima utimize wajibu wako stahili ndipo upewe haki yako stahili.
Leo tutaangalia namna kanuni za utoaji haki na mipaka yake kisheria pamoja na mawazo mbalimbali yaliyoongelewa na wasomi na wanasheria kwa kupitia kesi walizoamua na sababu za kishistoria za kanuni husika.
Maana ya Kanuni za utoaji wa haki,
Inaaminika wakati wa uumbaji wa ulimwengu katika kitabu cha Mwanzo Mungu alimuweka Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni ambapo aliwapa sheria ya kusogelea na kula matunda yote isipokuwa matunda ya mti wa katikati,Adam na mkewe walikiuka agizo hilo na hali wakijua kuwa wametenda kosa walijificha wasiuone uso wa Mungu,ile hali ya kujitambua kuwa wamefanya kosa na haikuwa ni sababu pekee ya Mungu kuwahukumu mpaka alipowapa nafasi ya kujieleza kuwa wamefanya nini na kwa nini(Fair hearing)ndipo Adam na Hawa walipo hukumiwa,huu ni ushahidi tosha kuwa ki asili haki hii ilianzishwa kitambo sana kabla wanadamu wengine hawakuwepo duniani,
wasomi wengi hasa wanasheria kutoka mataifa mbalimbali kwa muda tofauti wameelezea maana halisi ya utoaji haki kisheria, Mwanasheria Justice Jackson anaelezea kanuni hizi kuwa ni kutotenganisha mlolongo wa sheria na uwepo wa uhuru wa sheria na usawa bila ya upendeleo kwa maslahi binafsi,Lakini wengine kama Mwansheria Hamington J kutoka marekani anaelezea ni ule uwezo wa Kimungu uliomo ndani ya mwanadamu kutofautisha baya na zuri kwenye lengo la kuleta usawa katika jamii.
Ni kawaida kuwepo sheria katika taasisi zilizo za kiserikali na taasisi binafsi ambazo zitaleta nidhamu na ari na ufanisi wa kazi ikiwemo adhabu pale sheria au taratibu zinapokiukwa.
Sasa tuanze kuziangalia kanuni moja badala ya nyingine kwa kifupi sana na kuzielezea kanuni hizi za msingi wa utoaji haki duniani ambazo ni:
1)kanuni dhidi ya upendeleo(Rule agaist Bias)au kisheria inaitwa “Nemo Judex in Causa Sua”
Kanuni hii ina lengo la upatikanaji wa haki bila upendeleo katika ''mgogoro''inapotokea katika utatuzi wa mgogoro kukawa na upendeleo wa kimaslahi(Interest)mara zote hata utoaji wa haki usifanikiwe kwa kiwango kinachohitajika kuna sababu huweza kuchangia kuonekana kwa Upendeleo kama alivyoeleza Philip Philikunjombe katika kitabu chake cha sheria ya Utawala kuwa,kuhusiana kifamilia,au kuwa na maslahi ya mambo mbalimbali na wakati mwingine hata utegemezi wakiuchumi unawaweza kusababisha upendeleo katika mashauri.
2)Kanuni ya haki ya kusikilizwa(right of fair hearing)aun kisheria inaitwa ''Audi Alteram partem''
Kila mtu anayo haki ya kusikilizwa pale alipofanya kosa ikiwemo kujieleza ni kwa nini amefanya kosa, kama tulivyoona katika utangulizi wetu kuwa Adam na Hawa walipewa nafasi ya kusikilizwa walipotenda kosa na Mungu na kueleza ni kwa nini walitenda kosa,hata hivyo kutilia mkazo zaidi katika kesi ya R vs Cambridge Mahaka ilitoa amri ya kukataa uamuzi uliofanywa na chuo kikuu cha Cambridge baada ya mwanafunzi kufukuzwa chuo kutokana na utomvu wa nidhamu pqsipo kusikilizwa,kanuni hii inatoa amri kwa kila mtu kusikilizwa kwa haki pale alipokosea kisha adhabu ichukue mkondo wake pale kosa linapoonekana.
kanuni hii inatoa maelekezo kuwa mshitakiwa anatakiwa apewe taharifa ya kosa lake mapema kabla kuitwa kwenye shauri na hii imeonekana kwenye kesi ya Cooper vs. Wondsworth Board of Works (1963)14 CB ambapo kulikuwa na sheria ya kupewa notisi ya siku saba kabla ya kujenga mjini London uingereza lakini mdai wa hii kesi hakupewa notisi kwa muda wa siku saba na jengo lake lilibomolewa alipofika sakafu ya pili ya jengo,Mahakama ilihamuru uamuzi haukuwa sahihi kwa kuwa mdai wa shauri hakupewa muda wa kujiandaa kama sheria ilivyotaka na hakupewa haki ya kusikilizwa alipoomba kibali.
3)Sababu ya kufikia maamuzi ya shauri(A reason for Decision)
Ni lazima ielezwe sababu ya kufikia maamuzi ya shauri,je ni ni njia gani zimetumika kuleta suruhu na sababu zake.
HITIMISHO
Utoaji wa haki kisheria ni nadharia pana sana,na n somo refu sana,nimejaribu kuchukua angalau ya msingi katika kueleza,vipo vipengele vingine ambavyo ni vya muhimu pia lakini kutokana na rsilimali muda nimeamua kudadavua japo kwa kifupi tu ungalau msomaji upate mwanga wa namna haki inavyotolewa kwenye vyombo mbali mbali,nikutakie utulivu katika siku yako mpaka wakati mwingine panapo majaaliwa nitaendeleza mada hii kwa kuonesha utoaji wa haki katika mfumo wa mahakama za Afrika Mashariki! asanteni kwa kutembelea blog yangu!
No comments:
Post a Comment