Leo tutammulika mmiliki wa hii blog na mwanaharakati mchanga katika harakati za ukomboozi wa Taifa letu Tanzania,karibuni mumsome historia yake na hitikadi zake kupitia blog hii na sehemu hii ya ''tunayemmulika''
Karibuni sana!!!
Katika pitapita zangu ninatua mpaka Mwanza ambapo kuna chuo cha Mtakatifu Augustine,ninapiga kambi na kukutana kijana mwenye aibu kwa mtu mgeni anayekutana nae kwa mara ya kwanza na mwenye maneno mengi kila mara huku akizungumza kwa sauti kavu na yenye kusababisha kicheko kwa kila anayemsikiliza kwa ucheshi wake,mweupe na mrefu wa wastani na mwenye msimamo pale anaposisitiza kile anachokiamini.,tunapata wasaa wa kuzungumza nae na anaanza kufunguka kuhusu maisha maisha yake
Historia yake
Ilikuwa mchana wa tarehe 25 ya mwezi february ambapo mwanamke mmoja mjamzito alisikika akilia kwa uchungu huko kijiji cha Udoweni kata ya kawe Jijini Dar es salaam miaka 26 iliyopita,kipindi hicho kukiwa na umasikini mkubwa hakukuwa na barabara nzur ya kumuwahsha mjamzito hospitali na pamoja na kutokuwa na hospitali yenye ubora,mama hyuy aliwahishwa hospitali ya kijeshi Lugalo...anaanza kusimulia.
Wakati ninazaliwa ubora wa huduma za hospitali zilikuwa zi za kutosha na umeme ulikuwa wa kusuasua na ikitokea mama mjamzito yupo chumba cha kujifungua basi kuna uwezekano mkubwa mama na mtoto kupoteza maisha au mmoja wapo...anaongea kwa hisia.
Ndio hali iliyonitokea wakati nazaliwa siku ambayo Dr Balele alikuwa zamu na ilishangaza niliwezaje kuzaliwa kutokana na mazingira magumu kama yale,hivyo nilinusurika kifo siku ambayo nilikuwa nazaliwa,alisema Gerald.
Baba na mamaa kipindi hicho walikuwa hawana majina makubwa hivyo ilinilazimu kuishi maisha ya kawaida tena kwa wakazi wa kawaida hivyo nimepitia mazingira mengi mpaka hapa nilipofika.
Elimu yake
Nilianza elimu yangu ya awali mnamo mwaka 1993 Africa Sana kama shule ya awali na nilipofikisha miaka 7 nilianza Mwenge Shule ya msingi na sikukaa sana ilibidi nihamie Kawe ''A''shule ya msingi mwaka 1995-2000 ambapo nilimaliza darasa la saba mwaka huo.
Mwaka 2002 Nilianza elimu ya kati O-level Meta sekondari,walimu wangu wanasema nilikuwa mtundu sana na nilipenda kujaribujaribu Mambo na nikamaliza kidato cha nne mwaka 2005
Miaka miwili baadae baada mihangaiko mbalimbali ya mtaani nilijiunga Shule ya Sekondari Mbezi Beach ambapo nilianza kidato cha tano na kumaliza baadae.
Nilianza mbio katika siasa za Sekondari,nilipoingia sekondari kidato cha tano ilibidi acahuliwe Kaka mkuu na mimi nikasema nijaribu nafasi hiyo,nikachukua Form na kuijaza nikiwa na shabaha ya kuleta nabadiriko shuleni
Form zilirudishwa na nilipata pingamizi toka kwa mwalimu wangu wa darasa namkumbuka kwa jina la Mhilu,alisema hataki darasa lake litoe kiongozi yeyote kwa kuwa uongozi ni kupoteza muda wa masomo,nikashangaa sana,hivyo alikataa kujaza form yangu ya udhamini,sikukata tamaa na nilipeleka kwa walimu wengine wakaijaza na mbio zikaanza.
Tulikuwa watano kwenye mbio za Urais lakini bado nilikuwa mtu ninayeogopeka hata na wagombea wengine kwa sababu (1)walidhani nimetokea kwenye familia ya baba kiongozi wa nchi hivyo walidhani ninajua mambo mengi (2)waliogopa kwa sababu nilikuwa tayari nimejitangaza kwa O level kwenye watu wengi kuliko A level na mwisho wslihofia kwakuwa nilikuwa muongeaji sana hivyo nilipata marafiki karibu shule nzima wakati nilipojiunga na shule(kicheko)...kisha akanyamaza kwa muda
Kampeni zilianza na sikuwa nimejiandaa hivyo sikuwa na kampeni Manager kama walivyokuwa wenzangu akina Andrew Kerenge,Pia nilikuwa na Zablon Josam,Mathew Julius na Chunsi Ngogomba ambaye mimi baada ya kumaliza nasikia aligombe tena na akawa Headboy(Kicheko tena)
Siku ambayo sintoisahau kwenye kampeni ilikuwa ni siku nilipooingia Form Two D kulikuwa na mwalimu aliyekuwa anakwenda kuchapa wanafunzi nikaona hapohapo ndipo pa kuombea kura,nikawaambia mkinichagua nitakaaa na walimu waijadili upya hii adhabu ya viboko kuwa sio mara zote huwa inatibu kwa sababu ukimpiga mtoto wakati kakosa hesabu unachofanya ni kuubust mwili tu badala ya kumpa mwanafunzi mazoezi mengi yatakayofanya ukibust kichwa chake ambacho hakichaji,nilimaliza na kumuacha mwalimu aingie darasani ambapo yale maneno yangu yalimuudhi sana na sikujua kilichoendelea baada ya pale
Tulimaliza kampeni na siku ya matokeo yalitangazwa lakini pamoja na kupiga kampeni na kunadi wenzangu matokeo yangu hayakusoma vizuri,nikasema kulikoni?(aliongea kwa hisia)nikawa na uvumilivu kujua kulikoni,nikaja kuambiwa na bwana Daniel Zenda amabye sasa ni kiongozi wa chama(CCM)
(Bwana daniel zenda katika shughuli zake za kichama)
kuwa baada ya matokeo walimu walikaa kikao na kuamua waliyoamua kwa sababu sera zangu zilikuwa ni za kimapinduzi hivyo ningeleta shida,nikasema potelea mbali,wakanipa uwaziri mkuu wa shule kidogo nikatae nikasema wacha nichape kazi,nikakubali na kuanza kazi kama waziri mkuu(Special Duty Prefect cheo alichokuwa akishililia bwana Ahasan Kapalatu
Mgomo wa Shule
Katika kile ambacho walitabiri na kuja kutimia ni harakati nilizounga mkono baada ya msaidizi wangu na kiongozi mwenzangu kupigw makofi na mwalimu mmoja hivi huku kukiwa na fukuto la kuacha kazi mwalimu wa kiswahili(Mr Mhilu)huku tukikaribia kufanya mtihani wa taifa,tukaanzisha mgomo,huku viongozi tukisema tuna resign kwa kupigwa kiongozi mwezetu bila sababu wakati kiongozi alikuwa ndio mwenye ku dicpline shule,sasa leo anapigwa mbele ya mtu anayestahili kupewa adhabu,tukagoma tukianzia na Head Girl Angel Benard,tulivua beji zao na kuzirudisha ofisini kesho yake tukasimama assembly kama wanafunzi wa kawaida na sio viongozi tena
Walimu walituita na kueleza kero zetu kama viongozi na tuliytoa wiki moja ya kushughulikiwa matatizo yote ya wanafunzi ikiwemo kupewa mazoezi ya mara kwa mara yenye mfumo wa NECTA na ilikuwa hivyo mpaka tunamaliza.
Siasa za chuo kikuu(Saint Augustine University Mwanza)
Hivyohivyo chuo kikuu niligombea Uongozi wa darasa kwa tiketi ya Ubunge,ushindani ulikuwa mkubwa tangu siku ya mchujo na jina langu lilipita tena,yalipita majina mawili mimi na mgombea mwingine Hemeid Themith na kampeni zilianza na nikaibuka mshindi kwa kura 117 huku mwenzangu akiwa na kura 82 niawa mbunge wa darasa la sheria mwaka 2012/13 na nilikuwa mbunge wa kwanza wa darasa langu kumaliza muda wake wa uongozi kama mbunge,hata hivyo nilikuwa pia kwenye kamati nyingi kidogo za Bunge,nilikuwa kwenye kamati ya Nyumba na makazi na Kamati ya uchumi wa Bunge
Harakati na siasa a chuo kikuu ni ngumu kuliko zile za sekondari na inabidi utumie muda wako mwingi kutatua changamoto za wenzio
Siasa za nchi
Bado sijaona chama ambacho kimekuwa cha taifa kwa sasa,japo vipo vyenye misingi ya utu,kinachoonekana kwa sasa ni chama kushika hatamu kwa wingi kuliko uzalendo kwa sababu bado kuna vurugu la maslahi kwenye vyama vyetu na hili litaigharimu taifa
( Gerald na mdogo wake Claudia) Aidha Ikumbukwe pia Gerald J.Komba ni mtoto wa Kwanza kwa Mama yake bi Jane James Mkondya nani mtoto wa tano kati ya watoto 10 kwa Baba yake Mheshimiwa na Mbunge wa Mbinga magharibi kwa sasa ambapo wamezaliwa wawili yeye na mdogo wake Claudia kwa Mama yake
(Baba Mzazi wa Gerald)
Ana ndoto za kuwa mtu fulani na ndoto zake anaamini kuwa atakuwa mtoa haki kwa wakati akiitumia taaluma yake ya sheria
(Mama mzazi wa Gerald)
Wana blog hii wanamtakia mafanikio na kila la heri katika harakati zake za ukombozi huku wakimwambia mwanzo mzuri huleta mwisho mzuri kila la heri Bwana Gerald
No comments:
Post a Comment