Thursday, April 27, 2017
Zifahamu Dalili kuwa Ndoto zako zinakwenda Kufanikiwa
Kwa kawaida kila Mwanadamu huwa na matarajio ya namna anavyoweza kutimiza malengo yake,hizi zinaitwa ndoto.
Ndoto ni maono ya siku zijazo ambazo Mwanadamu anategemea zitakuwa kweli na zitadhirika katika ulimwengu unaoonekana.
Ndoto hizi au maono yako,zimegawanyika katika makundi mawili ambazo ni;
Long term dreams\long term plan,haya ni malengo ya mda mrefu ambayo mwanadamu anajiwekea,kwa mfano,ulishawahi kukaa na mtoto mdogo ukamuuliza baadae alikuwa angependa kuwa nani??wengine wanasema wanapenda kuwa madaktari,wengine wanapenda kuwa Maaskari,kila mtoto na malengo yake,hizi huitwa ndoto za mda mrefu,itachukua miaka mingi kuziona zikitumia.
Aina ya pili ni shirt plan dream\shirt plan,hii ni mipango ya mda mfupi,ambayo mtu amejipangia,mfano ushawahi kuona mfanyakazi anajipangia kufanya kazi kwa bidii ili aje kuwa mfanyakazi bora,aina hii ya ndoto huitaji maandalizi ya mda mfupi kutimia.
Sasa ili ndoto yako itumie,vipo vichocheo vinavyofanya ndoto itimie,naanza kuvitaja ili ulifahamu.
1.Ndoto inayokwenda kutimia ni lazima ipingwe:
Hii ni sifa kuu ya kwanza ya ndoto inayokwenda kutimia,utashangaa baada ya kuwaeleza watu ndoto yako,wapo watakaoipinga,mfano unakuta mtu ana kipato kidogo lakini ana mpango wa kufungua kampuni kubwa,sio kama uwezo hana wala vigezo hana,hapana,lakini wataibuka watu wa kumuambia hauwezi,japo ipo mifano mingi ya waliofanikiwa wakiwa na mitaji midogo au pengine hawakuwa na mitaji kabisa,kwa sababu tu,watu wanaolizunguka wameshaona wao hawakufanikiwa walipojaribu unachotaka kuliharibu,hivyo watakupinga.
2 Ni lazima ndoto yako itapata wafuasi:
Hawa ni wale watu watakaokutia moyo kuwa usiogope,wapo waliofanikiwa,wewe ni nani ushindwe,hawa watakutia nguvu na kukushauri pale unapokwama,wengi watakuweka karibu na kupenda kujua kupanda na kushuka kwako,changamoto unazopitia na watakuwa karibu nyakati zote.
3 Utasalitiwa:
Fahamu sio wote wanaokuja kwako na kukuambia tupo pamoja katika safari yako,hivyo wapo wapo wengine watakaokusaliti,ipo mifano mingi ya usaliti,biblia inawataja akina Yuda,utakaponiona hili usiogope,fahamu ndoto yako ina nguvu na ina uwezo mkubwa wa kufanikiwa.
4 Itakugharimu:
Ndoto inahitaji maandalizi na mipangilio,tegemea kutoa sadaka mda wako ili kutafuta uwezekano,utautumia mda wako kusoma waliofanikiwa katika eneo la ndoto zako,kama wewe unapenda siasa na haukubaliki,utajikuta kuna mda unatenga kusoma mbinu walizotumia watu wasiokubalika na wakashindwa,kama wewe ni mwanauchumi pia itajitahidi kujua waliofanikiwa wakiwa na kipato cha chini na wakafanikiwa,mda mwingine maandalizi ya gharama hugharimu pesa na vitu kama resources nyingine za kuifanya ndoto zako ziwe kweli.
5 Utapoteza Marafiki:
Unapotimiza ndoto zako kuna baadhi ya marafiki utawapoteza hasa wale watakaoingia katika kundi la kukupinga,kwa mfano unatamani kuwa mfanya biashara mkubwa,tegemea kuna marafiki ambao ulikuwa unatumia mda nao katika mambo mengine wataona amebadirika,hivyo watajiondoa wenyewe.
Mda mwingine inabidi ili uwe mtu wa ndoto flani flani,kuna makundi ya watu itabidi uachane nao ili kutengeneza sifa itakayokuletea ustawi,mfano huwezi kuwa na ndoto ya kuwa Mbunge au Rais wa taasisi iwapo ulio nao wanahakisi sifa zitakazokufanya watu wasiuamini,lazima uwakwepe na uanze kutafuta marafiki wapya wanaoendana na sifa ya ndoto zako.
6 Nitakuletea Connection ya watu:
Moja ya ndoto inayokwenda kutimia,utaanza kukutana na watu usiowategemea,ndoto inayokwenda kutimia huwa na tabia ya kukuunganisha na watu tofauti tofauti kwa urahisi zaidi,kwa mfano unatamani kuwa mwanasiasa mzuri,utashangaa unaanza kuwa na marafiki wengi wanasiasa ambao wana mafanikio nao wataanza kuzisikia habari zako,utashangaa wanaanza kuja siku hadi siku tunafahamiana na watu wengi ambao hukuwahi kufikiria,au unatamani kuwa mwanauchumi mzuri,utashangaa inakutana na watu waliofanikiwa hilo eneo na mnakuwa marafiki kwa mda mfupi,ukikiona hilo fahamu hiyo ndoto yako inakwenda kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
7 Ndoto itajitangaza yenyewe:
Ndoto huwa haijifichi,utashangaa watu wanaanza kujua hata bila ya kukitambulisha wewe ni nani kutokana na tunavyoongea,watu watajua ndani yako una ndoto kubwa,kwa mfano,mara nyingi watu wengi huniambia "wewe unafaa kuwa mwanasiasa" kwa nini,kwa sababu ya namna ninavyoongea na jinsi ninavyodadavua mambo,mwingine anakuuliza "una mpango wa kugombea popote?" na sio kweli kuwa ulijitangaza wewe ni mwanasiasa!!ni wao tu kwa kukusudia,wakajua ni nini unacho ndani,au mara nyingi unakuta mtu anakufananaisha na mtu fulani aliyefanikiwa moja kwa moja kutokana na misimamo yako,sio kama ulimwambia laa hasha kwa sababu ndoto huwa na tabia ya kujitangaza yenyewe.
8 Utakutana na mazingira yanayoipinga ndoto yako:
Hii ni dalili nyingine kuwa unaenda kufanikiwa,mambo yatakuwa magumu na mazingira ya kutimia ndoto yako yatakuwa magumu mno,hii ni kwa sababu ndoto ni kitu cha thamani,huwa kinapiganiwa ili akitumie,Fuatilia historia ya Baracj Obama,japo alikutana na ugumu wa maisha na alitoka katika familia ambayo huwezi kufikiria itatoa Rais wa Dunia lakini alikuwa na ndoto hiyo mda mrefu licha ya umasikini aliokuwa nao hapo hawali na ili uwe Rais wa nchi kubwa kama Marekani ni lazima uwe umejitosheleza kichumi.
Ukijitazama na kuitazama namna ndoto yako ilivyokuwa kubwa na mazingira unayekutana nayo ni tofauti,ujue hiyo ni ndoto inayokwenda kutimia punde.
9 Italeta ushindani:
Unaweza ukafikiria upo peke yako unayetafuta nafasi ya kutimiza malengo yako,lakini yupi mwingine nae anawaza kama wewe,kutumia fursa hizo hizo ulizowaza kuzitumia,inapokuja kwenye kutimiza malengo mnakutana,hapo ndipo huja "kivumbi na Jasho" hadi mwenye nguvu na akili kumzidi mwenzake ashinde,kwa kifupi,ndoto inayokwenda kutimia huwa na ushindani mkubwa tofauti na ndoto zisizo kwenda kutimia.
10 Ndoto huweza ikachelewa kutimia,hii ni sifa ya msingi,sio mara zote wengi huweza kwenda moja kwa moja kwenye kutimiza ndoto zao,wengine huchukua mda,wakaanguka na kuinuka tena,unapoona unashindwa kutimiza ndoto yako lakini ndani kunadai uendelee maana yake mda bado,unahitaji tujifunze zaidi na zaidi bila kuchoka,weka juhudi,fahamu nini kilikukwamisha alafu jaribu tena pasipo na kuchoka,sio wote wanapofanikiwa moja kwa moja na tunayo mifano.
Kwa kifupi,ndoto hupiganiwa,ndoto huchochewa ili ikue na kutimia,wengi walijaribu,hawakufanikiwa wakajaribu tena na tena,amini wewe ndio mwenye ufunguo wa hizo ndoto zako,usiruhusu mazingira au watu wakutoe kwenye ramani,jifunze kila siku changamoto zipo na lazima ukabiriane nazo!!
Usikate tamaa!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment